Sera ya Faragha ya S-BUSINESS
S-BUSINESS inaheshimu faragha ya watumiaji wake. Hii sera inaeleza kwa ufupi aina za taarifa tunazokusanya, jinsi tunavyotumia, na jinsi tunavyolinda taarifa zako.
Sera hii inaweza kubadilishwa mara kwa mara kadri tunavyoendelea kuboresha mfumo.
Kuhusu Sera ya Faragha
Tunajitahidi kulinda taarifa binafsi na taarifa za biashara ya kila mteja anayetumia S-BUSINESS. Taarifa hizi hazitumiki kwa njia nyingine nje ya madhumuni ya kutoa huduma ya mfumo wetu, isipokuwa pale sheria inapohitaji.
1 Data Tunazokusanya
Tunakusanya aina zifuatazo za taarifa ili kuweza kukupatia huduma zetu:
- Taarifa za akaunti: kama vile jina, barua pepe (email), namba ya simu, na taarifa nyingine unazojaza wakati wa usajili.
- Data za duka: bidhaa (products), mauzo (sales), stock, taarifa za wateja, suppliers, madeni, na taarifa nyingine za kibiashara unazoingiza kwenye mfumo.
2 Jinsi Tunavyotumia Taarifa
Taarifa zako zinatumika tu kwa madhumuni yafuatayo:
- Kutoa huduma ya mfumo: kuendesha POS, kusimamia stock, billing, report za mauzo, madeni ya wateja na suppliers, na vipengele vingine ndani ya S-BUSINESS.
- Kutuma arifa muhimu: kukujulisha mabadiliko ya mfumo, taarifa za usalama, taarifa za subscription, au taarifa nyingine muhimu zinazohusiana na akaunti yako.
3 Hifadhi & Usalama wa Data
Tunachukua hatua mbalimbali kulinda taarifa zako:
- Data huhifadhiwa kwenye database salama na tunatumia login na role-based access kuhakikisha kwamba kila mtumiaji anaona tu taarifa zinazomhusu kulingana na jukumu lake (admin, manager, salesperson, n.k.).
- Tunafanya udhibiti wa upatikanaji (access control) na hatua za kiusalama upande wa server kulingana na uwezo wa huduma yetu.
4 Maswali Kuhusu Faragha
Ukihitaji maelezo zaidi kuhusu sera hii ya faragha, unaweza kuwasiliana nasi kupitia ukurasa wa Contact, au kupitia taarifa za mawasiliano zilizopo ndani ya mfumo wa S-BUSINESS.